Kiongozi wa jimbo la Tigray, Debretsion Gebremichael amemtaka Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed kuyaondoa majeshi yake kwenye jimbo hilo, siku mbili baada ya Abiy kutangaza ushindi. 

Gebremichael amesema bado yuko karibu na mji mkuu wa Tigray, Mekele, ambao jeshi la Ethiopia siku ya Jumamosi lilisema linaudhibiti na amevishutumu vikosi vya serikali kuendesha ”kampeni ya mauaji ya kimbari” dhidi ya watu wa Tigray.

Akilihutubia Bunge jana, Abiy amesema wakati wanachukua udhibiti wa Mekele na miji mingine ya Tigray, wanajeshi hawajaua raia yeyote. 

Waziri wa Ethiopia anayehusika na demokrasia, Zadig Abraha amesema vikosi vya ulinzi vya serikali sasa vinaidhibiti Tigray na inaendelea na utaratibu wa kuwafikisha katika vyombo vya sheria viongozi wa waasi. 

Aidha, Abraha amesema nchi hiyo inapeleka misaada ya chakula kwa wakimbizi kupitia mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Laporta kuwania Urais FC Barcelona
Mdee: Hatuondoki CHADEMA

Comments

comments