Viongozi wa Arizona wameidhinisha ushindi wa Rais Mteule wa Marekani, Joe Biden ambaye ameshinda kura 11 za wajumbe baada ya kupata kura zaidi ya 10,000 dhidi ya Rais Donald Trump.

Biden (78), anakuwa Mgombea wa kwanza wa Urais kutoka Chama cha Democratic kushinda Jimbo hilo tangu mwaka 1996.

Aidha, Jimbo la Wisconsin nalo limemuidhinisha rasmi Biden kuwa mshindi na hadi sasa Trump ameshindwa katika majimbo yote sita ambayo aliomba matokeo kurudiwa upya akilalamikia udanganyifu.

Viongozi wa Arizona wamesisitiza kuwa Uchaguzi Mkuu wa Novemba 3, 2020, ulifuata Sheria.

KARATE yapelekwa Ruvuma
Biden aandika historia nyingine Marekani

Comments

comments