Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, ameutaka uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kwa kushirikiana na Wakala wa Barabara (TANROADS), kusimamia kikamilifu maboresho ya miundombinu katika kiwanja cha Ndege cha Arusha kwa mujibu wa mkataba na taratibu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Anga – ICAO, ili kuwezesha Ndege kubwa kutua.

Ameyasema hayo wakati akikagua maboresho yanayoendelea kwenye kiwanja hicho, amesema kwa kufanya maboresho hayo pia itasaidia hata pato la Taifa kukua.

Hata hivyo Serikali imewekeza jumla ya Shilingi Bilioni 11 kwa ajili ya kufanya maboresho ya miundombinu katika Kiwanja cha hiyo, pia ni Kiwanja ni kati ya viwanja vitatu vya ndege nchini, vinavyopokea idadi kubwa ya ndege na abiria kwa siku, kikiongozwa na viwanja vya ndege vya Dar es Salaam na Mwanza.

“Kiwanja hiki ni kinaingizia Serikali fedha nyingi kutokana na upokeaji wake wa idadi kubwa ya watalii hivyo hakikisheni mnasimamia kikamilifu maboresho haya sambamba na kuboresha huduma kwa wateja wenu ili ndege nyingi zaidi ziendelee kutua katika Kiwanja hiki,” Amesema Naibu Waziri Kasekenya.

Naye Meneja wa TAA mkoa wa Arusha, Mhandisi Elipigi Tesha, amemuambia Naibu Waziri Kasekenya kuwa hadi sasa maboresho yaliyokwishafanyika yamegharimu kiasi cha shilingi Bilioni Tano 5, ambapo kazi zilizofanyika ni uongezaji wa barabara za kuruka na kutua ndege mita 200 na kufika urefu wa mita 1,860 na kutawezesha ndege nyingi zaidi kutua kwenye kiwanja hicho.

Mhandisi Kasekenya amemaliza ziara ya kikazi ya siku mbili jijini Arusha, kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Serikali inayosimamiwa na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.

Tanzania, Kenya kuunda mfumo wa kushirikiana kiutalii
Waziri Ummy: tutekeleze maagizo ya Rais Samia