Mdau wa Soka mkoani Tanga Nassor Bin Slum ameitahadharusha Young Afrivans kwa kuitaka ijipange kuelekea mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’.

Coastal Union imejihakikishia kucheza Fainali ya michuano hiyo leo Jumapili (Mei 29), baada ya kuichapa Azam FC kwa changamoto ya mikwaju ya Penati 6 kwa 5, katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Bin Slum ambaye aliwahi kuidhamini Coastal Union ametoa tahadhari kwa Young Africans, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook, dakika chache baada ya mpira kumalizika jijini Arusha.

Bin Slum ameandika: “Yanga mjipange tunakuja, This is New Coastal Union under Guardiola Mnene…..Kama wewe ni shabiki wa Mangush piga keleleee”

Young Africans ilitangulia Fainali jana Jumamosi (Mei 28), kwa kuifunga Simba SC 1-0 jijini Mwanza Uwanja wa CCM Kirumba.

Mchezo wa Fainali utapigwa Julai 02 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambao leo Jumapili (Mei 29) umetumika kwa mchezo wa Nusu Fainali.

Mkuu wa mkoa afichua siri nzito Coastal Union
Azam FC chalii, Coastal Union yaifuata Young Africans