Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (Fifa), Joseph ‘Sepp’ Blatter amekataa kujiuzulu nafasi yake licha ya wadhamini wakuu kumtaka afanye hivyo mara moja kutokana na kashfa za ufisadi.

Coca-Colla, Visa, Budweiser na MacDonald wote wametoa matamko yao rasmi wakimtaka mzee Blatter kujiuzulu baada ya kufunguliwa mashtaka ya jinai nchini kwake Uswiz wiki moja iliyopita.

Katika tamko lao, Coca-Cola wasema, “Kadri siku zinavyoenda ndivyo taswira na heshima ya Fifa inazidi kuharibika.” Nao MacDonald wao wamesema kuwa kuondoka kwa Blatter kutakuwa njia sahihi zaidi ya kuuokoa mchezo wa mpira wa miguu duniani.

Wiki iliyopita, Muendesha Mashtaka wa Uswiz alimfungulia mashtaka mzee Blatter mwenye umri wa miaka 79 kwa madai ya kusaini mkataba usioifaidisha Fifa pamoja na kubariki malipo ya ‘magumashi’ kwa rais wa Uefa, Michel Platini.

Hata hivyo, Blatter alikana tuhuma hizo.

 

 

Lowassa Amng’ang’ania Mgombea Ubunge Wa Monduli CCM
NEC Yapiga Marufuku NCCR-Mageuzi, CUF Kusimamia Kura Za Lowassa