Aliyewahi kuwa kiungo wa klabu nguli za barani Ulaya FC Barcelona na AC Milan, Kevin-Prince Boateng amejiunga na klabu ya Monza inayoshiriki Ligi daraja la kwanza nchini Italia (Serie B).

Boating amejiunga na klabu hiyo inayomilikiwa na Waziri Mkuu wa zamani wa Italia Silvio Berlusconi, ambaye pia aliimilikia klabu ya AC Milan, akitokea na Fiorentina.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka amesaini mkataba wa mwaka mmoja, lakini atakua na uhuru wa kuboresha mkataba huo endapo atahitaji kufanya hivyo katika kipindi chote atakachokuwa klabuni hapo.

Boateng amewahi kucheza soka kwenye klabu ya Besiktas ya Uturuki, Tottenham Hotspur, Portsmounth (England) na Schalke 04 (Ujerumani).

Kevin-Prince ni ndugu wak beki wa ambingwa wa Ujerumani FC Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani, Jerome Boateng.

Datavision International yasherehekea miaka 22 ya mafanikio
Papa Francis akataa kuonana na waziri wa Marekani

Comments

comments