Kundi la kigaidi la Boko Haram limewaonya wasichana zaidi ya 100 lilowateka na kuwaachia hivi karibuni kuhakikisha hawarejei tena shuleni kuendelea na masomo.

Kundi hilo ambalo moja kati ya itikadi zake ni kupinga elimu yenye mfanano na ile ya magharibi, liliwateka wasichana hao Februari 19 katika shule ya bweni eneo la Dapchi nchini Nigeria.

Jumla ya wasichana 110 walitekwa na kundi hilo, watano walifariki walipojaribu kutoroka na mmoja ameendelea kushikiliwa kutokana na msimamo wake wa kutobadili dini.

Wasichana waliorejeshwa kutokana na makubaliano kati ya kundi hilo na Serikali ya Nigeria wamewekwa chini ya uangalizi maalum wakifanyiwa uchunguzi wa afya zao.

Wazazi wa watoto walioachiwa wakifurahia kukutana tena na binti zao

Aidha, wasichana hao pamoja na wazazi wao wanatarajiwa kukutana na rais Muhamadu Buhari.

Gambo awashauri Chadema kushirikiana na Serikali
UVCCM yaweka wazi sababu za kutenguliwa Jokate