Kiungo Mario Gotze atakosa mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya 16 bora utakaoshuhudia Borussia Dortmund wakipapatuana na Benfica baadae hii leo.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, anaendelea kuuguza jeraha la mguu ambalo lilimnyima nafasi ya kucheza mwishoni mwa juma lililopita, katika mchezo wa ligi ya nchini Ujerumani  dhidi ya Darmstadt waliokubali kibano cha mabao mawili kwa moja.

Wachezaji Marcel Schmelzer na Lukasz Piszczek, ambao pia walikosa mchezo dhidi ya Darmstadt, wanatarajia kujiunga na wachezaji wenzao wa Borussia Dortmund katika mchezo wa hii leo ambao utachezwa mjini Lisbon nchini Ureno.

Kwa upande wa wenyeji, mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Argentina Eduardo Salvio ana matumaini ya kucheza, kufuatia kupona majeraha ya kifundo cha mguu.

Hata hivyo mshambuliaji wa kibrazil Jonas yupo shakani kucheza dhidi ya Borussia Dortmund, baada ya kukosa mazoezi ya jana.

Kuelekea katika mchezo wa usiku wa leo, Dortmund watakua na nafasi nyingine ya kuhakikisha wana waridhisha mashabiki wao, kufuatia hali yao ya kupata ushindi kutoridhisha tangu mwezi Disemba mwaka jana, kwani wamefanikiwa kushinda michezo miwili kati ya michezo minane.

Pep Guardiola: Tunasubiri Majibu Ya Vipimo
CAF Yaichimba Mkwara COSAFA