Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari anarejea nyumbani mara baada ya kukaa kwa zaidi ya siku 100 Jijini London alikokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa ambao haukutajwa.

Taarifa kutoka Ofisi ya Rais Nchini humo zimesema kuwa, Buhari alitarajiwa kurejea nyumbani Jumamosi jioni mara baada ya kutibiwa na kupata nafuu Jijini London, ambapo anatarajiwa kulihutubia taifa kupitia vyombo vya habari.

Aidha, Rais huyo ambaye ni Jenerali mstaafu amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya kiafya tangu mwezi Juni mwaka jana, lakini tangu aanze kusumbuliwa na matatizo hayo bado ugonjwa wake haujawekwa hadharani.

Hata hivyo, kwa upande wao Wapinzani wakuu wa Buhari katika uchaguzi wa mwaka 2015 uliomuingiza madarakani wamedai kuwa Rais huyo anasumbuliwa na saratani ya tezi dume, kitu ambacho mwenyewe amekikanusha.

 

Naibu waziri ajiuzulu kwa kashfa ya kumpiga mwanamke
Andrea Barzagli: Juvuntus Hatutoyumba