Zaidi ya Shilingi 11 Bilioni zinatarajia kutumika
kupitia Miradi ya Mikataba 7 ukiwemo wa P4R na Kemondo Maruku, kufanikisha upatikanaji wa Maji safi na salama Wilaya Bukoba, Kagera ili kuondoa adha ya uhaba wa hitaji hilo kwa Wananchi.

Akizungumza na Dar24 Media Meneja wa Wakala ya Usambazaji Maji na Usafi na Mazingira Vijijini – RUWASA Wilaya Bukoba, Mhandisi Evaristo Mgaya amesema Programu ya Lipa kwa Matokeo (P4R), inatekeleza jumla ya miradi sita ya Mikataba yenye thamani ya Bolioni 3.2
itakayowanufaisha Wananchi 3,570 kwenye Wilaya hiyo.

Amesema, “fedha zake zinatolewa na wafadhili kutoka World Banck na Mradi huu mkubwa wa Kemomdo Maruku unaoendelea kutekelezwa na serikali ya Tanzania unajengwa katika awamu mbili, awamu ya kwanza umefikia asilimia 90 na kwa awamu ya pili inayoendelea kutekelezwa katika kata tatu umefikia asilimia 55.”

Aidha, Mhandisi Mgaya ameitaja miradi inayotekelezwa na P4R kuwa ni Mradi wa Kasharu uliokamilika na umeanza kutoa huduma kwa Wananchi na ule wa Kikomelo Butakya ambao ujenzi wake umekifika asilimia 75 ambapo miundombinu ya Mabomba ya kilomita 28 inajengwa pamoja na vituo 20 vya kutolea huduma ya maji.

Mwingine ni mradi wa Bumai uliopo Kata ya Bugabo, unaotekelezwa ambao umefikia asilimia 65, Migara iliyopo kata ya Rubale uliofikia asilimia 38 na ule wa Mshozi uliopo Kata ya Kaagya unatelelezwa kwa gharama ya bilioni 1.4 na umefikia asilimia 97 ukitoa huduma kwa njia ya Majaribio.

Hata hivyo, Mhandisi Mgaya amesema Shughuli zote hizo zinalenga kuifikia asilimia 85 ya utoaji wa huduma ya maji Vijijini, ili kufanikisha azma ya Serikali ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa Wananchi.

Vijana watakiwa kuzitambua fursa za kiuchumi
Baraza la Wafanyakazi lapeleka furaha PURA