Na Allawi Kaboyo-Bukoba.

Naibu katibu mkuu wizara ya maji mhandisi Nadhifa Kemikimba ameiagiza mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Bukoba (BUWASA), kuhakikisha ifikapo juni 2021 iwe imesambaza mtandao wa maji katika manispaa ya Bukoba kwa asilimia 100% kutoka asilimia 88% za sasa.

Kemikimba  ametoa agizo hilo kwa niaba ya Katibu mkuu wa wizara hiyo katika hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya BUWASA iliyofanyika   Bukoba mjini na kuitaka BUWASA kuhakikisha usambazaji wa maji kote katika mji wa Bukoba ili wakazi wake kupata maji kwa ukaribu zaidi.

kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, wadau na watumiaji wa maji pamoja na watumishi wa BUWASA.

“Tunaelewa kuwa malengo yetu ni kuwa ifikapo  2025 usambazaji wa maji mijini iwe imefikia asilimia 100% lakini kwa Bukoba ni mbali  sana, haiwezekani kila mwaka tunasema tumefikia asilimia 88% ya usambazaji wa maji wakati hapa kila kitu kipo na kinapatikana, maji yapo  tena ya kutosha mtakapokwama tuambieni lakini napenda ifikapo Juni 2021 usambazaji uwe umefikia asilimia 100% na si vinginevyo,” amesema Kemikimba.

Aidha ameitaka bodi mpya ya BUWASA kuweka mikakati ya kuwa na miundombinu madhubuti  kuzuia maji kuvuja jambo ambalo limekuwa likisababisha hasara kwa mamlaka na kuitaka bodi hiyo kufuatilia madeni ya wateja ili yalipwe kwa wakati.

Sambamba na hilo, BUWASA imetakiwa kusimamia mapato na Matumizi ya Mamlaka ikiwa ni pamoja na kuwaondoa wale wote waliovamia vyanzo vya maji ili kuzuia ukosefu wa maji hapo baadae.

Serikali kupitia Wizara ya Maji imetenga takribani Bilioni 7.2 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo BUWASA ni Wasimamizi ikiwemo miradi ya Kayanga Omurushaka, Upanuzi wa mtandao wa usambazaji Maji ndani ya Manispaa ya Bukoba, Mradi wa Maji Miji mikuu minne ya Wilaya ambayo ni Biharamulo, Kyaka Bunazi, Muleba na Ngara na Miradi mingine.

"Kila sekunde 30 mtu mmoja anajiua kutokana na tatizo hili la afya ya akili" - Katibu mkuu UN
Nigeria: Aliyewanyonga wanawake tisa ahukumiwa kifo