Mbunge wa Bunda Mjini kupitia tiketi ya (CHADEMA), Ester Bulaya amesema kuwa uwezo wa wabunge wa CHADEMA kwa wanawake ni mkubwa mno ukilinganisha na uwezo wa wabunge wanawake wa CCM na kusema kuwa Mbunge mmoja wa CHADEMA ni sawa na wabunge 100 wa CCM.
Ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa na kituo kimoja cha Televisheni nchini Kenya alipokwenda kumtembelea na kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye anapatiwa matibabu kufuatia kupigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017.
“Tanzania wanawake wa upinzani tuna uwezo zaidi kuliko wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kabisa, sisi tuna msemo wetu kwamba Mbunge mmoja wa CHADEMA ni sawa na wabunge 100 wa Chama Cha Mapinduzi na hiyo ni kauli ya Mwenyekiti wetu, Freeman Mbowe, sasa ukiona wabunge wengine wageni bungeni hawana uzoefu, wamekuja na wanataka kupata umaarufu anafanya vioja sisi wazoefu ambao tumepambana na kushindana na wakongwe wa kwenye chama hicho tunampuuza,”amesema Bulaya
-
CCM wampongeza aliyekodi ndege ya Lissu
-
Lissu ampa ujumbe mzito Zitto, ‘Tumeshinda’
-
Msigwa amvaa Musukuma, amtaka aache kulalamika
Hata hivyo, mbali na hilo, Bulaya ameongeza kuwa amemkuta Mbunge Tundu Lissu akiwa anaendelea vyema na kusema amempa ujumbe kwa Watanzania kuwa wajiandae