Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga, amewaonya viongozi, taasisi za umma na wananchi wanaoshiriki katika kupindisha sheria na mipango mbalimbali ya maendeleo inayoandaliwa na serikali kuacha tabia hiyo mara moja.

Mkuu huyo wa Mkoa ametoa onyo hilo katika uzinduzi wa mpango kabambe wa Maendeleo ya Manispaa ya Kigoma Ujiji wa mwaka 2017 mpaka 2037 uliowasilishwa kwa wadau wa maendeleo.

Amesema ili mpango huo kabambe wa maendeleo uweze kuleta tija, ni lazima watu wabadilike kifikra na kuona kuwa maendeleo ya mkoa muhimu kuliko maslahi ya mtu mmoja mmoja.

Kwa upande wake Afisa Mipango miji wa kampuni ya CRM Land Consult Tanzania Limited, ambayo inashughulika na mipango miji na vijiji, Evarist Mfinanga amesema tofauti na mipango ya huko nyuma ambayo haikuwa na ushirikishwaji, mpango huo wa 2017 mpaka 2037 utakuwa na mafanikio makubwa.

Gharama zinazokadiriwa kukamilisha mpango kabambe wa maendeleo ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, ni zaidi ya shilingi trilioni 3

David Unsworth atamani kuwa kocha mkuu Everton
Bulaya: Mmoja CHADEMA sawa na mia CCM