Everton watakutana na Chelsea usiku wa leo katika kombe la Qarabao Cup, mchezo huu utakuwa wa kwanza tangu walipomfukuza kocha Ronald Koeman na timu hiyo kuwa chini ya kocha wa muda David Gerald Unsworth

David Unsworth ambaye ni kocha wa muda wa Everton amesema kuwa anatamani kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo kwani ni klabu kubwa yenye mashabiki wazuri na kila kocha angependa kuifundisha klabu hiyo.
“Ni kazi ngumu sana, unajua tulipo sasa lakini ni lazima tupambane na kurejea katika kiwango chetu, ninaamini tuna wachezaji wazuri wakiongozwa na Rooney na tuna nafasi ya kurejea katika kiwango chetu,” alisema David Unsworth.
Kocha huyo ameongeza kuwa mwenyekiti wa klahu hiyo pamoja na bodi ya klabu tayari wamempa nafasi ya kuonyesha uwezo wake kwa kuisadia klabu kupata matokeo mazuri jambo ambalo litaamua hatma yake katika klabu hiyo.
Kocha wa Burnley Sean Dyche na kocha wa zamani wa Bayern Munich Carlo Ancelotti wote wanahusishwa na kutaka kumrithi Ronald Koeman ambaye ametimuliwa baada ya kipigo cha mabao 5-2 ambacho Everto ilikipata kutoka kwa Arsenal.

Video: Serikali haikununua ndege bila mpango mkakati- Eng. Matindi
RC Kigoma awataka wananchi wabadilike