Serikali imekusanya zaidi ya Shilingi Milioni 200 baada ya kuwapiga mnada ng’ombe walioingizwa kinyemela kutoka nchi jirani ya Kenya na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira.

Hayo yamesemwa hii leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpiga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa wizara yake imejipanga na kuendelea na oparesheni maalum ya kukamata na kuondoa mifugo yote inayovamia kutoka nchi jirani kupitia mikoa ya mipakani.

Ameitaja mikoa hiyo ya mpakani ambayo imekuwa ikivamiwa ni Katavi, Kigoma, Tanga, Mara, Ruvuma, na Arusha na kuagiza wakuu wa mikoa na wilaya kuendesha opresheni hizo Maalum ndani ya siku saba.

“Mimi, Naibu waziri wangu, makatibu wakuu na wataalam tunaingia tena katika opareshi hiyo maalum kesho.” amesema Mpina

Aidha, ameongeza kuwa serikali haipo tayari kuingia gharama ya kutibu magonjwa yanayoletwa na mifugo wanaovamia kutoka nchi jirani ambao kwa namna moja au nyingine huleta uharibifu wa mazingira kwa kukata miti hovyo, kusababisha mmomonyoko wa udongo na kuchangia kwa kiasi kikubwa migogoro ya wakulima na wafugaji.

Hata hivyo, ameongeza kuwa mifugo ya Tanzania inatakiwa kuwa na chapa huku akisema suala hilo linashughulikiwa ili kuweza kuondoa mkanganyiko ambao unaweza kujitokeza.

Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 25, 2017
Video: DC Mjema aingilia kati ugomvi wa FFU na wananchi jijini Dar