Bunge nchini Burundi limepitisha muswada wa sheria uliowasilishwa na Waziri wa Sheria, kuruhusu polisi kufanya ukaguzi katika makazi ya watu bila kibali maalumu.

Waziri wa Sheria nchini humo Aimé Laurentine Kanyana ameutetea muswada huo kwa kile alichokitaja kuwa Burundi kwasasa inakabiliwa na matukio ya mauaji ya kikatili, ugaidi, bishara ya binadamu na kumiliki silaha kinyume cha sheria, utumiaji wa dawa za kulevya na ubakaji.

Aidha, Vyama vya upinzani nchini humo, vimehofia utaratibu huo, ambapo mkuu wa chama cha upinzani, UPRONA , Abel Gashatsi amesema kuwa muswada huo wa kuruhusu watu wasakwe majumbani usiku na polisi ni hatari.

Kwa upande wa chama kikongwe cha upinzani, FRODEBU kimesema kuwa muswada huo unakiuka katiba na kupendekeza baraza la Seneti kuurejesha na kuipinga.

Hata hivyo, kuna uwezekano mkubwa wa muswada huo kutopata pingamizi lolote bungeni, kwa sababu ya idadi kubwa ya wajumbe wa chama tawala cha CDD-FDD.

 

Makamanda Boko Haram wajisalimisha
Korea Kaskazini yatangaza kuachana na makombora ya nyuklia