Chama cha soka nchini England (FA) kimepanga ratiba ya michezo ya mzunguuko wa tatu wa michuano ya kombe la ligi (Carabao Cup) itakayochezwa Septemba 25.
Katika ratiba hiyo majogoo wa jiji Liverpool wamepangwa kucheza na Chelsea, katika uwanja wa Anfield.
Wawili hao watakutana mara mbili mfululizo katika juma moja, ambapo baada ya mchezo huo, Chelsea watawakaribisha Liverpool kwenye uwanja wa Stamford Bridge, kwa ajili ya mpambano wa ligi Septemba 29.
Ratiba hiyo inaonyesha, mabingwa watetezi wa michuano hiyo Manchester City wamapangwa kupambana na Oxford United wanaoshiriki ligi daraja la pili nchini England.
Katika hatua nyingine, meneja Jose Mourinho atakutana kwa mara ya kwanza na mchezaji wake wa zamani Frank Lampard akiwa mkuu wa benchi la ufundi la Derby county kwenye uwanja wa Old Trafford.
Lampard alicheza chini ya utawala wa Mourinho alipokua meneja wa klabu ya Chelsea na kufanikiwa kutwaa taji la ligi ya England mara mbili mfululizo msimu wa 2004/05 na 2005/06.
Washindi wa pili wa michuano hiyo msimu uliopita Arsenal wamepangwa kuanzia nyumbani Emirates Stadium kwa kuwakabili wapinzani kutoka jijini London, Brentford.
Tottenham watakua wenyeji wa Watford, na tayari wameshawasilisha maombi kwenye bodi ya EFL, ili mchezo huo upigwe kwenye uwanja wa MK jijini London.
Everton watacheza dhidi ya Southampton na Wolves watakutana na Leicester City.
Ratiba kamili ya michezo ya mzunguuko wa tatu wa michuano ya kombe la ligi (Carabao Cup).
West Brom v Crystal Palace
Arsenal v Brentford
Burton v Burnley
Wycombe v Norwich
Oxford United v Manchester City
West Ham v Macclesfield
Millwall v Fulham
Liverpool v Chelsea
Bournemouth v Blackburn
Preston v Middlesbrough
Wolves v Leicester
Tottenham v Watford
Blackpool v Queens Park Rangers
Everton v Southampton
Manchester United v Derby
Nottingham Forest v Stoke