Hatimaye tunaona mradi wa kwanza wa video wa Rich Mavoko tangu alipojiondoa kwenye lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), hatua ambayo imezua mgogoro wa kimkataba.

Mavoko jana ameachia video ya ‘Ndegele’ ambayo imepikwa na muongozaji maarufu wa video za muziki nchini, Adam Juma wa Visual Lab, lakini kuna dalili kuwa video hiyo imewakwaruza Wasafi.

Video hiyo inaanza na igizo fupi, inaonesha kikundi cha watu ambao ‘wamteka’ mtu mmoja ambaye anaonekana kuwa na taharuki akihoji anapelekwa wapi, huku akihowahoji pia kama wao ni wale watu wasiojulikana.

Mtu huyo ambaye alionesha uoga anatambulishwa kwa jina la ‘Msafi’ na mrembo ambaye anaonesha hali ya ubabe, “kelele za nini? Tuliza kend* hapo. Umekuta watu wako kwenye party umekuja kufanya vurugu. Wewe si ni ‘Msafi’?”

“Mimi ni Msafi ndiyo,” anajitambulisha kijana huyo kwa sauti ya unyonge kidogo. “Sasa wewe kama ni Msafi, leo unakutana na ‘Wachafu’ tena wachafu kwelikweli,” anajibu dada mbabe.

Mwanzo huo hautakuacha na jibu la haraka hadi utakapokuwa unaendelea na video hiyo. Mwisho utaunganisha matukio kuona kuwa kijana huyo alianzisha vurugu akitaka kumshambulia Mavoko aliyekuwa amewasha moto wa ‘Ndegele’.

Kilichomkuta kijana huyo Msafi anajua ‘Bwana Dairekta’.  Angalia video hapa:

Afisa Elimu, Mkuu wa shule kibeta wasimamishwa kazi
Carabao Cup: Liverpool kuikabili Chelsea