Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedua Jenerali Marco Elisha Gaguti ameagiza Mratibu wa Elimu wa kata ya Kibeta Hashim Upunda, Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kibeta Enetha Isdory na Msaidizi wake Sundi Elisha kusimamishwa kazi pamoja na kuivunja kamati ya shule hiyo.

Hatua hiyo ni kufuatia kwa mwalimu mkuu kushindwa kudhibiti nidhamu ya walimu  jambo ambalo limekuwa kichocheo cha mauaji ya kikatili yaliyomkuta mwanafunzi wa darasa la tano Spelius Eradius yaliyofanywa na mwalimu Respicius Patric aliyedaiwa kumfanyia mwanafunzi huyo mauaji hayo baada ya kumtuhumukuwa ameiba mkoba mwalimu Elieth Gerald.

Brigedia Jenerali Gaguti ametoa agizo hilo alipofika shuleni hapo baada ya kukutana na walimu na wanafunzi katika shule.

Akizungumza amesema walimu hao watakuwa nje ya kazi ili wapishe uchunguzi wa kamati aliyoagiza iundwe na uongozi wa Manispaa ya Bukoba kwa lengo la kuchunguza vitendo  vinavyodaiwa kukithiri katika shule vya walimu kutoa adhabu kwa wanafunzi bila kufuata taratibu.

Hofu yatanda kundi la paka kushiriki mazishi Lindi
Video: Mavoko aachia video ya Ndegele, awakwaruza WCB