Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo kwa nyakati tofauti, amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa chama tawala cha Burundi (CNDD-FDD) Reverien Ndikuriyo na Balozi wa Namibia nchini Lebius Tangeni Tobius.
Mazungumzo hayo yemefanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM Dodoma.
Aidha katika mazungumzo yake na Chongolo, Katibu Mkuu huyo wa chama cha CNDD-FDD amesifu uhusiano mzuri uliopo kati ya chama hicho na CCM na amesisitiza kuuendeleza na kuendelea kujifunza kupitia uzoefu mzuri wa uongozi ndani ya CCM.
Wakati wa mazungumzo hayo Chongolo amemuhakikishia Ndikuriyo kuwa, CCM itaendelea kuimarisha uhusiano mzuri uliopo na kuendeleza mshikamano, urafiki na undugu wa kihistoria na CNDD-FDD.
Wakati wa mazungumzo yake na Balozi wa Namibia nchini, Lebius Tangeni Tobius, viongozi hao wameahidi kuendelea kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Namibia pamoja na chama tawala cha Namibia (SWAPO) na CCM.