Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linamshikilia Mohamed Mussa maarufu kama Kibosile kwa madai ya kuwa tapeli sugu ambaye amekuwa akighushi nyaraka mbalimbali bandia za Serikali na ambazo sio za Serikali kwa kutumia mihuri mbalimbali na kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.

“Vitendo hivyo vimekuwa vikichafua taswira ya Serikali, amekamatwa na mihuri mbalimbali 24, vyeti vya kuhitimu sekondari, vyeti vya masomo ya sekondari, vyeti vya hati za tabia njema za Jeshi la Polisi, vibali vya uraia kwa wageni nchini, mihuri ya Taasisi za Serikali na binafsi kama Wizara ya Mambo ya Nje, UDSM, Manispaa ya Ilala, CRDB, NMB, STANBIC BANK, Rita, Wanasheria, Maafisa Watendaji, Polisi na Idara mbalimbali” amesema Muliro.

Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linamshikilia mtuhumiwa sugu wa kughushi nyaraka za taasisi na serikali Mohamed Mussa Mohamed maarufu kama Kibosile akiwa na hati za kusafiria zaidi ya 130.

Kamada Muliro ameeleza kuwa mtuhumiwa huyo pia amekamatwa pia na kadi za benki mbalimbali 16, Scanner 2 za kughushi nyaraka, hati mbalimbali za kusafiria (Passport) 33 za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Mbali na vitu hivyo, Mohamed Mussa (Kibosile), amekamatwa akiwa na hati za kusafiria zaidi ya 130.

Mtuhumiwa huyo anaendelea kuhojiwa kwa kushirikiana na Taasisi nyingine na atafikishwa Mahakamami taratibu zitakapokamilika.

Aidha, Jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa wengine zaidi ya 15.

CCM, CNDD-FDD bega kwa bega
Askari elfu 34 kupandishwa vyeo