Chama Cha Mapinduzi CCM kimepanga kupambana na umasikini kikamilifu katika kipindi cha miaka mitano iyajo endapo wanachi watakipa tena ridhaa ya kuongoza serikali ya awamu ya tano.

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira ameyasema hayo jana mjini Musoma alipokuwa akiwahutubia wanachama wa chama hicho katika uwanja wa Mukendo.

Wasira ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Bunda anaemaliza muda wake, alieleza kuwa CCM inatambua kuwa zaidi ya asilimia zaidi ya 28 ya watanzania wanaishi katika hali ngumu ya umasikini na kwamba idadi kubwa zaidi ni ya wale wanaoishi vijijini, hivyo wamejipanga vyema katika kipindi kingine cha miaka mitano kubadili hali hiyo.

“Wengi wa hawa wanaishi kijini na wanalima kwa jembe la mkono. Tumeazimia kupambana katika miaka mitano ijayo, kupambana kadiri tunavyoweza kuhakikisha tunapunguza umasikini,” alisema Wasira.

Mgombea ubnge (CCM) Musoma Mjini, Vedastus Mathayo akiwa na wafuasi wake mjini humo

Mgombea ubnge (CCM) Musoma Mjini, Vedastus Mathayo (Katikati) akiwa na wanachama wa chama hicho

Umasikini ni moja kati ya maadui wakuu watatu wa Taifa hili waliotangazwa na Mwalimu Julius Nyerere katika awamu ya kwanza. Lakini licha ya kufanyika jitihada nyingi kuutokemeza, bado wananchi wa Tanzania wameendelea kuishi katika hali ya umasikini kwa zaidi ya miaka 50 huku nchi ikiwa na  tajiri ya maliasili.

Sera ya kuutokemeza umasikini inaonekana kuwa moja kati ya karata muhimu zaidi inayochezwa na chama Tawala na vyama vya wapinzani katika kuomba ridhaa ya watanzania kuunda serikali ya awamu ya tano.

 

Lowassa Amsemea Kingunge
FC Barcelona Si Lolote Kwa Athletic-Bilbao