Kikosi cha Athletic-Bilbao usiku wa kuamkia hii leo kilikamilisha shughuli ya kutwaa ubingwa wa Spanish Super Cup kwa mwaka 2015, baada ya kulazimisha matokeo ya sare ya bao moja kwa moja dhidi ya mabingwa wa Ulaya, FC Barcelona.

Athletic-Bilbao, walilazimisha matokeo hayo wakiwa ugenini mjini Barcelona kwenye uwanja wa Camp Nou, huku wakisaidiwa na ushindi wa mabao manne kwa sifuri waliouvuna kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita.

Matokeo hayo yameiwezesha Bilbao kupata ushindi wa jumla wa mabao matano kwa moja.

Lionel Messi, alitangulia kuipatia bao Barcelona katika dakika ya 43 kipindi cha kwanza lakini Aritz Aduriz aliharibu shughuli kwa kufunga bao la kusawazisha dakika ya 75.

Mchezo huo ulishuhudia beki wa kati wa Barcelona Gerard Pique akitolewa nje ya uwanja kufuatia adhabu ya kadi nyekundu sawa na Kike Sola wa Bilbao mwishoni mwa mchezo.

CCM: Tunaujua Vizuri Umasikini Wa Watanzania
Azam FC Kurejea Dar Leo