Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa amezungumzia uamuzi wa UVCCM kumvua Ukamanda Mkuu ngazi ya Taifa, kada mkongwe wa chama hicho, Kingunge Ngumbale Mwiru.

Lowassa ndiye aliyetajwa kuwa moja kati ya sababu za UVCCM kumvua madaraka hayo mzee Kingunge kutokana na ukaribu wa wawili hao hasa wakati wa mbio za kuwania nafasi ya kugombea urais kupitia chama hicho, alilaani uamuzi huo.

Akiongea jana katika mkutano mkubwa wa hadhara visiwani Zanzibar, Lowassa alieleza kuwa amesikitishwa na uamuzi huo wa CCM kwa kuwa wamesahau mchango mkubwa wa mzee Kingunge katika chama hicho.

Edward Lowassa na Kingunge Ngombale Mwiru enzi zile

Edward Lowassa na Kingunge Ngombale Mwiru enzi zile

Alieleza kuwa Kingunge alikuwa msemaji mkubwa wa CCM katika masuala ya uchumi na kwamba aliwasaidia kuvuka katika ngazi mbalimbali za mabadiliko. Alisitiza kuwa bila Kingunge chama hicho kisingefika hapo kilipo.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Katibu Mkuu wa UVCCM, Sixtus Mapunda alitoa taarifa kwa vyombo vya habari akieleza kuwa UVCCM ilifanya mkutano na kuamua kumvua Kingunge Ngombale Mwiru Ukamanda Mkuu kwa kuwa amebainika kwenda kinyume na maadili na taratibu za chama. Ukaribu wake na Edward Lowassa na kauli zake alizozitoa baada ya jina la swahiba wake huyo kukatwa na Kamati Kuu, ni kati ya sababu zilizotajwa.

Man Utd Mtegoni Barani Ulaya
CCM: Tunaujua Vizuri Umasikini Wa Watanzania