Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameeleza kusikitishwa na hatua waliyoichukua wabunge wa Kambi ya Upinzania kwa kutowasalimia wala kushiriki nao vyakula.

Wabunge hao wamesema kuwa hali hiyo imevuka mstari wa uhasimu wa kisiasa na kuanzisha uadui, hivyo kuna haja ya kukaa na kuzungumza ili mambo mengine ya Bunge yaweze kuendelea kati yao.

Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini, Hilary Ngonyani maarufu kama Profesa Maji Marefu amesema kuwa alimshuhudia Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa akiikataa salamu ya Mbunge wa Viti Maalum, Anna Lupembe (CCM), kitendo ambacho amekilaani vikali.

“Mambo yanayofanyika Zanzibar wanatuletea Bungeni, wamejitoa katika magrupu hata ya WhatsApp ambayo mara zote tumekuwa tukifahamishana nini kinaendelea na kujadili vitu kwa pamoja,” alisema Maji Marefu.

Naye Mbugne wa Mafinga, Cosato Chumi (CCM) alieleza kuwa kile kinachofanywa na wabunge wa Upinzani ni utoto na kwamba yatashuka hadi kwa wananchi.

Msigwa ambaye ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje,  waliazimia kutoshirikiana na wenzao wa CCM wakidai kuwa wamekuwa wakiwasilisha masuala ya msingi Bungeni lakini wenzao wamekuwa wakiwapuuzwa hivyo wameamua kuchukua hatua zaidi.

Uledi:Michango ya Mifuko ya Hifadhi ya jamii tutaipeleka kwa wakati
Linex: Arvil na Jokate mimi siyo type yao