Kiungo wa klabu ya Chelsea Cesc Fabregas ameendelea kupingana na baadhi ya vyombo vya habari vinavyomuhusisha na mpango wa kukata kuihama klabu hiyo kabla ya dirisha kufungwa usiku wa kuamkia Septemba mosi mwaka huu.

Fabregas amekanusha uvumi huo ambao uliibuka kufuatia taarifa za kutokua na maelewano na meneja wa Chelsea Antonio Conte, ambaye ameonyesha kumuweka katika hali ya sintofahamu kuhusu mustakabali wake wa soka huko Stamford Bridge.

Fabregas alianzishwa katika kikosi cha kwanza kati kati ya juma lililopita wakati wa mchezo wa kombe la ligi (EFL Cup) dhidi ya Bristol Rovers, lakini imekua tofauti katika michezo ya ligi kuu ya soka nchini England ambapo mpaka sasa amecheza mchezo mmoja tena akiingi kama mchezaji wa akiba dhidi ya Watford.

Mwishoni mwa juma lililolpita hakucheza kabisa licha ya kuwa katika orodha ya wachezaji wa akiba, hali ambayo imeendelea kuzua hofu na mashaka kwa watu wake wa karibu, kufuatia taarifa zinazoendelea kuripotiwa dhidi yake.

Hata hivyo alipoulizwa Fabregas katika mahojiano maalum na kituo cha Sky Sports, alijibu hana wasiwasi na changamoto zinazomkabili na hajawahi kufikiria kama ataondoka klabuni hapo.

“Sina wasiwasi na yanayoandikwa kuhusu mimi, najua haya ni mapito na mambo yatakuja kukaa sawa, na sijawahi kumwambia meneja kama nataka kuondoka,”

“Natambua uwajibikaji wangu nikiwa hapa, na ninajua ipo siku nitarejea katika mipango ya meneja ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha Chelsea.” Alisema Fabregas.

Shkodran Mustafi Afichua Siri Ya Kuwa Mshika Bunduki
MTV VMAs: Drake afunguka jukwaani ‘anavyomzimia’ Rihanna