Drake amevunja ukimya katika jukwaa la tuzo za  video za MTV (MTV VMAs) akieleza jinsi anavyompenda Rihanna tangu akiwa na umri wa miaka 22.

Rapa huyo toka Toronto Canada, ambaye alichaguliwa kumkabidhi RiRi tuzo ya ‘Michael Jackson Vanguard 2016’, alisema kuwa amekuwa akimpenda Rihanna na kumuangalia kama mfano ingawa yeye ni mdogo wake.

“Ni mtu ninayempenda tangu nikiwa na umri wa miaka 22. Ni rafiki yangu kipenzi dunia nzima. Katika maisha yangu yote ya utu uzima, nimekuwa nikimuangalia yeye kama mfano, ingawa ni mdogo zaidi yangu,” alisema Drake kabla hajamuita jukwaani Rihanna na kumkabidhi tuzo hiyo.

Wawili hao walijua kucheza na macho ya watazamaji ambao waliripuka kwa shangwe baada ya Drake kufunguka ya sakafu ya moyo wake.

Walisogelea mithili ya njia na kinda wanaotaka kubadilishana vyakula mdomoni, lakini ghafla walikwepa na kupeana ‘kumbatio’ la mahaba.

Drake na Rihanna MTV VMAs

Tetesi za mapenzi kati ya wawili hao zimeendelea kuwa kizungumkuti. Huku matukio yao yakionesha kuwa walishawahi kudatishana na kuzama kwenye kisima cha mapenzi hadi kupelekea ugomvi mkubwa kati ya Drake na Chris Brown aliyekuwa mpenzi wa zamani wa RiRi.

Cesc Fabregas Aendelea Kukanusha Uvumi Wa Kuihama Chelsea
Finca yapongezwa kwa kupunguza gharama za ukopaji.