Kiungo wa kati wa Chelsea Cesc Fabregas amesema wachezaji wa Chelsea wanaolipwa mishahara mikubwa wanafaa kucheza kama wachezaji nyota.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi ya Premia wamedorora sana msimu huu na wamo nafasi moja juu ya eneo la kushushwa daraja baada ya kushindwa Jumatatu ugenini Leicester.

Baada ya mechi hiyo, meneja wa Chelsea Jose Mourinho alisema juhudi zake zilisalitiwa na baadhi ya wachezaji.

“Ikiwa wewe ni mchezaji nyota, na unalipwa kama mchezaji nyota, unafaa kucheza kama mchezaji nyota na kujibeba kama mchezaji nyota,” kiungo wa Uhispania Fabregas amesema.

“Sisemi kwamba huwezi kuwa na msimu mbaya na mechi mbaya lakini mtazamo lazima uwe ule ule.

“Lazima tusalie kucheza vyema mechi zetu, na tabia yetu inafaa kuwa tofauti na tunayoona sana kwa kila mchezaji wa Chelsea.”

Ashinda Udiwani Kwa Tiketi ya Chadema akiwa gerezani
Lowassa kuanza ziara ya Nchi nzima Kesho