Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema akiungwa mkono na vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa, Edward Lowassa ataanza ziara ya kuzunguka nchi nzima kuanzia kesho kwa lengo la kuwashukuru wapiga Kura.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene imeeleza kuwa kesho (Disemba 17) Lowassa ataanza ziara hiyo mkoani Tanga akiambatana na viongozi wa juu wa Chadema na Ukawa.

Katika taarifa hiyo, Makene alieleza kuwa Lowassa atawashukuru wananchi kwa kura nyingi walizompigia yeye na wagombea ubunge na udiwani wa Ukawa, kura zilizowezesha kupata viti vingi bungeni na kuongoza Halmashauri 34 nchini.

“Wananchi wanastahili shukrani kwa imani hiyo kubwa ambayo ni ishara ya wazi kuwa matumaini yao kwa miaka mingine mitano yatasimamiwa na kuongozwa na upinzani imara kupitia Ukawa, ” alisema Makene.

Katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu, Lowassa alishika nafasi ya pili baada ya kupata asilimia 39.9 ya kura halali akimfuatia Dk. John Magufuli aliyeshinda baada ya kupata asilimia 58.4.

Cesc Fabregas Awageuka Wachezaji Wenzake
Mrithi Wa Andrey Coutinho Asaini Mwaka Mmoja Yanga