Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), jana kililazimika kuondoa Katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, hati ya mashtaka dhidi ya Jeshi la Polisi kupinga kuzuiwa kwa mikutano ya kisiasa nchini.

Jaji wa Mahakama hiyo, Mohammed Gwae aliwaambia waandishi wa habari kuwa Chadema waliridhia kuondoa hati ya mashtaka dhidi ya Jeshi la Polisi baada ya kukubaliana kuwepo mapungufu katika hati hiyo. Alisema mapungufu hayo ni kumjumuisha Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Nsato Mssanzya ambaye kisheria anatakiwa kufunguliwa kesi katika Masjala Kuu (Main Registry).

“Tulishauriana na mawakili wa Chadema kuhusu mapungufu hayo, waliamua kwa hiari yao kuondoa kesi yao kwa ajili ya kuifanyia marekebisho hati yao ya mashtaka,” Jaji Gwae.

Hata hivyo, Jaji Gwae alieleza kuwa Chadema wanayo nafasi ya kufanya marekebisho na kuwasilisha mashtaka yao katika mahakama hiyo baada ya kuliondoa jina la Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Nsato Mssanzya au kufungua kesi hiyo katika Masjala Kuu.

Wanasheria wa Chadema, John Mallya na Paul Kipeja walikiri kuondoa shtaka hilo kwa muda na kwamba watalifanyia marekebisho na kulirejesha ili kesi hiyo ianze kusikilizwa kwani tayari imeshapangiwa Jaji.

Chadema walifungua kesi mahakamani hapo kupinga agizo la Polisi, ikiiomba Mahakama hiyo kuagiza kuwa agizo la Jeshi hilo ni batili na kuwataka Polisi walinde mikutano ya vyama hivyo. Katika kesi hiyo, wanawastaki wakuu wa polisi wa wilaya za Maswa, Kahama na Geita pamoja na    Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Nsato Mssanzya.

Lusinde: Wabunge wa Chadema wameniomba nimwambie Mbowe asiwaburuze, ni dikteka
Lowassa amuamkia IGP Mangu