Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya jamii zikidai kuwa kamati kuu ya chama hicho imempitisha kuwania nafasi ya Ubunge jimbo la Monduli Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa

Kamati Kuu ya (CHADEMA), imekutana katika kikao chake maalum jana Jumatano Agosti 15, 2018 kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali kuhusu chama hicho na taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Chadema mkoa wa Arusha, Amani Golugwa ambapoi amesema kuwa taarifa za kuteuliwa Lowassa hazina ukweli wowote kwani kufanya hivyo ni kumshusha hadhi Waziri Mkuu huyo mstaafu na kudai kuwa hadhi yake kwa sasa ni nafasi ya urais.

“Hayo sio mapendekezo ya kamati kama wanavyosema na hizo ni taarifa za uzushi na zinafanywa na wapinzani wetu kutaka kutuchafua, hakuna mgombea aliyepitishwa na mapendekezo yote yaliyotolewa ni ya awali,” amesema Golugwa.

Hata hivyo, Fred ambaye ni mtoto wa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, alichukua fomu ya kuwania ubunge jimbo hilo wiki iliyopita lakini jana aliomba kujiondoa kwakile alichodai kuwa bado muda wake muafaka licha ya kuonekana kuungwa mkono na wanachama wengi awali.

 

 

Utafiti wa LHRC wabaini wafanyakazi wengi hawazijui haki zao
Ainsley Maitland-Niles nje mwezi mmoja na nusu