Diwani wa kata ya Ubungo, Boniface Jacob (Chadema) amechaguliwa kuwa Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo katika uchaguzi uliofanyika leo.

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo, Jacob aliyekuwa akiungwa mkono na vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa alipata jumla ya kura 16 kati ya kura 18 za wajumbe wote, akimshinda Yenga (CCM) aliyepata kura 2.

Kwa upande wa Naibu Meya, Kwangaya Ramadhani (CUF) alichaguliwa kwa kupata kura 15 kati ya kura 18, akimshinda Abdul Lema (CCM) aliyepata kura 3.

Awali, Jacob alikuwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni ambayo iligawanywa na kupelekea madiwani kugawanyika na yeye kuhamishiwa Halmashauri hiyo mpya.

Lema, Mkewe watua mikononi mwa polisi kwa uchochezi, lugha za kuudhi
Wakala wa majengo Tanzania waanza kutimiza ahadi za Rais Magufuli