Uongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)kimesema hakitambui majina 19 ya wambunge kwenye nafasi ya viti maalumu ambao wamekula kiapo siku ya leo Novemba 24, Bungeni Dodoma.

Akizungumza na Dar24 Katibu wa chama hicho , John Mnyika amesema kuwa kilichofanyika ni kinyume cha katiba ya na maamuzi ya kamati kuu ya CHADEMA.

“Si maamuzi ya chama chetu, kamati kuu haijawahi kukaa wala kupeleka majina kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wala bunge,waulizeni tume ya uchaguzi orodha imepelekwa na nani” amesema Mnyika.

Aidha john Mnyika amesema kuwa CHADEMA itafanya maamuzi baada ya kikao cha kamati kuu kukaa na kuja na azimio.

BOFYA HAPA.

Trump asalimu amri kwa Biden
Wabunge 19 viti maalum CHADEMA waapishwa

Comments

comments