Kiungo Mshambuliaji kutoka Zambia Clatous Chotta Chama amerejea jijini Dar es salaam na kujiunga na wenzake kambini, tayari kwa mchezo wa Mzunguuko wa sita wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi Dodoma Jiji FC.

Simba SC itakuwa mwenyeji wa mchezo huo, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, huku ikichagizwa na kambi ya visiwani Zanzibar, ambako ilicheza michezo miwili dhidi ya Kipanga FC na Malindi FC.

Chama ambeya kwa sasa amekua chachu ya ushindi wa kikosi cha Simba SC kila anapopewa nafasi ya kucheza, alienda Zambia kwa matatizo ya kifamilia, katika kipindi cha kupisha michezo ya Kalenda ya FIFA.

Kikosi cha Simba SC kilirejea jijini Dar es salaam jana Alhamis (Septemba 29), kikitokea visiwani Zanzibar, huku Kocha Mkuu wa Muda Juma Mgunda akithibitisha kuridhishwa na maandalizi waliyoyafanya visiwani humo.

PICHA: Tembo Warriors waendelea kujifua Uturuki
Masau Bwire aitambia Young Africans