Uongozi wa klabu ya Azam FC umekiri kuanza mazungumzo na Kocha Kali Ongala ili ajiunge na kuanza kukifindisha kikosi chao.

Azam FC imemtimua kocha  Zeben Hernandez raia wa Hispania pamoja na jopo zima alilokuwa akiliongoza.

Lakini kwa sasa kikosi chao kitanolewa na Iddi Cheche na Iddi Aboubakary wakati mazungumzo na Majimaji kumng’oa Kali yakiendelea.

 Kocha wa muda wa Azam FC Iddi Cheche mwenye jezi namba 17

Cheche ni mmoja wa makocha wa timu ya vijana ya Azam FC.

Hata hiyo uongozi wa Azam FC umekiri kutarajia kuwa na kocha wa kigeni kwa siku za usoni .

Taarifa zimeeleza, Azam FC imefanya mazungumzo na Lamine N’Diaye aliyewahi kuifundisha TP Mazembe na timu ya taifa ya Senegal.

Video: Majaliwa ahimiza kilimo, 'wanaotaka fedha wataipata shambani'
Mussa Mapunda: Tumepata ITC Ya Ngassa