Msanii wa Hip Pop, Chid Benz siku chache zilizopita alizungumza na kutoa ushauri kwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimtaka kufanya vitu vichache ili kuhakikisha anavikamilisha na kuachana na kufanya mambo mengi ambayo baadae yatampa lawama.

”Naona Makonda angerelax angefanya vitu vichache kwanza avikamilishe vichache vile ambavyo vimemuweka kwenye kile kiti anachokikalia now, kuliko kumix muziki michezo serikali kutamchanganya na hata akijaribu kufanya vitu vyote kwa pamoja akidhani nguvu hiyo anayo sidhani kama nguvu hiyo anayo maana mi ofisisni kwake napajua” amesema Chid.

”Makonda asifanye vitu ambavyo baadae vitampa lawama, unajua watu wengine wanakusubiri umalize ule ukiti wako ndio waanze kukupa lawama ni suala zuri aliloliamua lakini asibase sana kwenye wasanii watu wa michezo” Chid.

Chid amesema ni vyema Makonda angesaidia mambo mbalimbali ya kijamii kama vile kuhakikisha hospitali kuna dawa za kutosha, vituo vya daladala kujengewa vizuri ili abiria kujikinga na mvua pamoja na jua, lakini pia Chid amegusia suala la gereza la Segerea akidai kuwa lina hali mbaya hivyo angeona namna ya kufanya marekebisho, pia ametaja suala la kuondoa watu kariakoo ili kuruhusu magari kupita vizuri.

”Nafikiri angestiki kwenye masuala ya kuondoa watu karikaoo magari yapite vizuri angestiki kwenye mitumba watu siku hizi wanajua karume lakini watu hawapapendi, angejua pale mabanda yanafanyeje labda mule ndani pangekuwa na mashine za pesa, angefanya utaratibiu wa mahospitali kuhusu madawa yawepo sana kusiwe na complain kuhusu madawa, angefanya uwezekano wa vituo vya daladala vijengwe kwa namna fulani labda vikajengewa watu wasipigwe na jua wala kunyeshewa na mvua”Chid.

Ameongezea ”Angedeal na vituo vya polisi, naona kulivyo angeenda Segerea kule ajue Segerea kunatengenezwaje, chini watu wanalalaje, sababu hata yeye anytime anaweza kwenda, watu wamejisahau, kule kuna hali mbaya sana, kule hata Magufuli akimaliza urais anaweza akaenda kama anamatatizo, so afadhali ujitengenezee mazingira ya kule kama unajijua sio mazuri yeote unayoyafanya” .

Chid amesema hayo pindi alipofanya mahojiano na media ya PRO24 ambapo alihojiwa juu ya suala lililoletwa na Makonda la kukopesha wasanii, ambapo alihojiwa akipata nafasi ya kupata mkopo angefanyia nini.

Chid amesema ni vyema Mkuu wa Mkoa Makonda angekuwa anafanya vitu fulani vya nchi kuliko kujihusisha na watu wa michezo na muziki akiamini kuwa wataweza kumpigia kelele.

”Sisi dakika ya mwisho huwa tunatakaga hela” amemalizia Chid.

 

Video: Fahamu sababu ya vilema hivi kupendwa na watu wengi zaidi duniani
Nape amtaja Lowassa, 'Huyu ni rafiki yangu mkubwa'