Beki wa klabu ya Reading inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini England Chris Gunter, amemaliza utawala wa mshambuliaji wa pembeni wa mabingwa wa soka barani Ulaya Real Madrid Gareth Bale, kwa kutangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Wales.
Bale alikua anashikilia rekodi ya kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo kwa miaka minne iliyopita, kufuatia mafanikio aliyoyavuna akiwa na timu ya taifa pamoja na kikosi cha Real Madrid ambacho kimetwaa ubingwa wa Ulaya mara mbili tangu mwaka 2014.
Hata hivyo mshambuliaji huyo amatajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka kwa kupigia kura na wachezaji wa soka wa Wales, huku kiungo wa Stoke akitajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka kwa kupigiwa kura na mashabiki.
Mwanadada Laura O’Sullivan ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Wales, Angharad James amekua mchezaji bora wa mwaka kwa kupigiwa kura na wachezaji wenzake huku Jess Fishlock akipigiwa kura na mashabiki na kutangazwa kuwa mshindi wa mwaka 2017.
Ben Woodburn na Peyton Vincze wametangazwa kuwa wachezaji bora wa mwaka mwenye umri mdogo.
Katika hatua nyingine tuzo ya heshima ya mwaka 2017 ya chama cha soka nchini Wales, imekwenda kwa aliyekua mshambuliaji wa timu ya taifa ya nchi hiyo na klabu ya Liverpool Ian Rush.
Tuzo za wachezaji bora wa Wales kwa mwaka 2017 (WANAUME).
Mchezaji bora wa mwaka: Chris Gunter
Mchezaji bora wa mashabiki: Joe Allen
Mchezaji bora mwenye umri mdogo: Ben Woodburn
Mchezaji bora wa vyombo vya habari: David Edwards
Mchezaji bora wa wachezaji: Gareth Bale
Tuzo ya heshima ya chama cha soka nchini Wales (FAW): Ian Rush
Mchezaji bora wa ligi kuu ya soka nchini Wales: Craig Williams – Newtown AFC
WANAWAKE.
Mchezaji bora wa mwaka: Laura O’Sullivan
Mchezaji bora mwenye umri mdogo: Peyton Vincze
Mchezaji bora wa wachezaji: Angharad James
Mchezaji bora wa mashabiki: Jess Fishlock