Mshambuliaji wa klabu bingwa nchini England Chelsea Alvaro Morata, huenda akawa nje ya uwanja kwa zaidi ya mwezi mmoja, kufuatia majeraha ya misuli ya paja aliyoyapata wakati wa mchezo wa ligi mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Man City.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye alijiunga na Chelsea kwa ada iliyoweka rekodi klabuni hapo ya Pauni milioni 60 akitokea Real Madrid, kwa sasa anaongoza ka upachikaji mabao miongoni mwa wachezaji wa The Blues.

Madaktari wa timu ya taifa ya Hispania wamemfanyia vipimo mshambuliaji huyo mara alipowasili kwenye kambi ya timu hiyo inayojiandaa na michezo ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia, na wamebaini Morata analazimika kupumzika kwa ajili ya kufanyia matibabu.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na madaktari wa kikosi cha Hispania, yamebainisha kuwa majeraha ya mshambuliaji huyo huenda yakachukua muda wa majuma manne ama zaidi ili kupona kabisa.

Hispania watacheza dhidi ya Albania na Israel.

Hispania inaongoza msimamo wa kundi G kwa tofauti ya point tatu dhidi ya mabingwa wa dunia wa mwaka 2006 timu ya taifa ya Italia Italia, ambao pia wamesaliwa na michezo miwili.

Kwa mantiki hiyo, Morata hatakuwa sehemu ya kikosi cha Chelsea kitakachorejea dimbani Oktoba 14 kucheza dhidi ya Crystal Palace, kisha kupapatuana na AS Roma kwenye mshike mshike wa ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Michezo mingine ambayo Morata ataikosa itakua dhidi ya Watford na Everton.

JPM awataka wakurugenzi ‘waokoke’, kuvunja makundi
Chris Gunter amaliza utawala wa Gareth Bale