Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Collins Opare, amekamilisha mpango wa kujiunga na Klabu ya Dodoma Jiji FC katika kipindi hiki cha Dirisha la Usajili, kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Opare ametimkia kwa ‘Walima Zabibu’, akitokea Biashara United Mara yenye maskani yake makuu mjini Musoma mkoani Mara, iliyoshuka Daraja mwishoni mwa msimu uliopita 2021/22.

Kiungo huyo amekamilisha taratibu za kujiunga na Dodoma jiji FC, baada ya kumalizana na Uongozi wa Biashara United Mara, ambao unajiandaa kushiriki Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao 2022/23.

Opare ameondoka Biashara United Mara kama Mchezaji huru na amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Dodoma Jiji FC.

Kwa sasa mchezaji huyo yupo jijini Dar es salaam kwa mapumziko binafsi, siku kadhaa zijazo anatarajiwa kuelekea mkoani Dodoma kuanza maisha yake mapya.

Sakata la Katiba mpya, Viongozi upinzani wawekwa kizuizini
Serikali yawatanguliza wakulima hatua moja mbele