Kesi inayomkabili askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima jana ilipelekea chup* yake kuoneshwa mbele hakimu mkazi wa mahamaka ya Kisutu, Cyprian Mkeha.

Nguo hiyo ya ndani ilitolewa kama kielelezo cha ushahidi baada ya wakili wa erkali Jacline Nyantoli na Shadrack Kimaro kueleza kuwa ni sehemu ya vielelezo vinavyoonesha kuwa begi lilipelekwa mahakamani hapo ni mali ya mshitakiwa anaekabiliwa na kesi ya kushindwa kuhifadhi silaha na risasi, kinyume cha sheria.

Pamoja na nguo hiyo ya ndani, vitu vingine vilivyotolewa kwenye begi la Askofu Gwajima ni suruali mbili, soksi, makoti mawili, bastola aina ya Berretta na risasi 17, CD mbili, chaja ya simu, hati ya kusafiria, vitabu na leseni ya kumiliki silaha.

Hatua hiyo ilifikiwa mahakamani hapo baada afisa wa Polisi idara ya upelelezi alijitambulisha kwa jina la Sospeter kutoa ushahidi wa kina kuhusu kesi hiyo na kutaka kutambua mmiliki wa begi lilifikishwa mahakamani hapo.

Baada ya kusikiliza ushahidi huo na kuwapa nafasi upande wa mshatikiwa kuuliza maswali, Hakimu Mkeha aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 6 mwaka huu.

Lowassa: CCM Wananizushia, Waandae Maelezo Tukiingia Ikulu
Unachopaswa Kufanya Katika Hatua Za Awali Za Uhusiano Na Msichana Unaempenda