Kiungo wa Klabu ya Dodoma Jiji FC Cleophace Mkandala amewaaga Viongozi, Wachezaji na MAshabiki wa wa klabu hiyo, baada ya kumaliza msimu wa 2021/22, huku klabu hiyo ikiendelea kuwa miongoni mwa vilabu vitakavyopambana Ligi Kuu msimu ujao 2022/23.

Mkandara aliyedumu kwa miaka mitatu kwenye kikosi cha Dodoma jiji FC ametuamia Ukurasa wake wa Instagram, kuwaaga wachezaji wenzake, ikiwa ishara ya kuondoka klabuni hapo katika kipindi hiki cha Dirisha la Usajili.

Kiungo huyo ameandika: Nichukue Nafasi Hii Kumshukuru Mungu Mwingi wa Rehema Kwa kumaliza ligi msimu huu Salama….

Awali ya yote nitoe Shukran Zangu za Dhati kwa uongozi mzima wa timu yangu ya Dodoma jiji FC Viongoz, Wachezaji, Pamoja na Mashabiki kwa kipindi tulichopo pamoja…

Sinabudi Kuwaaga ndugu zangu pale nilipowakosea kuwakwaza Mnisamehe Kibinaadamu nitawakumbuka kwa nyakati zote (Nyumbani) Niwatakie Muendelezo mwema katika mpira wa miguu.. Asanteni

Taarifa zinaeleza kuwa, Kiungo huyo tayari ameshamalizan na Azam FC ya jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuwatumikia msimu wa 2022/23, ambao utaanza rasmi mwezi ujao (Agosti).

Simba SC kurejea Dar es salaam leo
TPLB yaanika mkeka wa Play Off