LeBron James ameisaidia Cleveland Cavaliers kuibuka na ushindi wa point 93-89 dhidi ya Golden State Warriors alfajiri ya leo, na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa NBA kwa msimu wa 2015-16.

Ushindi huo unaifanya klabu ya Cleveland Cavaliers kuishinda Golden State Warriors katika michezo minne mfululizo miongoni mwa michezo saba waliyocheza kwa majuma mawili.

Katika michezo mitatu ya awali Golden State Warriors, walifanikiwa kuibuka kidedea na kuonyesha huenda wangetetea taji la NBA ambalo walilitwaa mwaka 2015 kwa kuwafunga Cleveland Cavaliers.

TFF Waushangaa Uongozi Wa Stand Utd Kampuni
Ajira Zaidi ya 500 Kuwanufaisha Wahitimu Elimu ya Juu