Zaidi ya watoto wa mtaani 2,000, wakiwemo 205 kutoka nchi jirani wameokolewa na serikali nchini Senegal tokea mlipuko wa virusi vya corona ulipoingia nchini humo.

Akitoa taarifa hiyo jana, Katibu mkuu wizara ya wanawake, familia na jinsia, Mame Gor Diouf amesema wameokoa watoto walio na umri kati ya mika 4 -17, na miongoni mwao watoto 1,219 wamerudishwa katika familia zao.

Amesema kuwa kati ya hao zaidi ya watoto 50 wameambukizwa virusi vya corona na wanapatiwa huduma katika vituo vya afya na miongoni mwao tayari wamepona.

Serikali nchini Senegal imeanzisha operesheni maalum kuwalinda watoto ambao wapo kwenye mazingira hatarishi kipindi hiki cha ugonjwa wa Covid 19.

Hadi sasa nchi hiyo imethibitisha visa 1,492 vya waathirika wa virusi vya corona, vifo vitatu na waliopona 562

Mume wa Mwimbaji Jennifer Mgendi afariki dunia
Mwakalebela: Tumelipokea kwa furaha tamko la Rais