Mshambuliaji Cristiano Ronaldo ameendelea kuchukua nafasi kubwa katika vyombo vya habari juma hili, ikiwa ni muendelezo wa kauli aliyoitoa mara baada ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Real Madrid kwa miaka mingine mitano.

Ronaldo alizungumza na waandishi wa habari siku ya jumatatu na kueleza mipango yake ya kutaka kucheza soka kwa miaka kumi ijayo, akiwa katika kiwango kama ilivyo sasa.

Ronaldo amesema angependa kumaliza soka lake akiwa na klabu iliyomkuza na kumtambulisha katika ulimwengu wa soka duniani Sporting Lisbon ya nchini kwao Ureno.

Amesema anaamini mpango huo utafanikiwa kutokana na ukaribu uliopo kati yake na mashabiki wa klabu hiyo ambayo ilikubali kumuuza mwaka 2003, ambapo alijiunga na Man Utd.

Image result for cristiano Ronaldo in Sporting Lisbon on sky sportsCristiano Ronaldo alipokua Sporting Lisbon

Ronaldo amebainisha kuwa, anatambua upo ukomo wa kuitumikia Real Madrid na huenda mkataba wa miaka mitano aliousaini mwanzoni mwa juma hili ukawa wa mwisho kwake klabuni hapo.

“Itakua vizuri kwa upande wangu kumalizia soka nikiwa nyumbani Ureno, nitapenda kujiunga na klabu iliyonikuza na kukithamini kipaji changu, hadi ikafikia hatua ya kila mmoja dunia kunitambua.

“Najua siku hiyo itafika na itakua ni furaha hata kwa rafiki zangu wa karibu ambao tulikua sote na kukuzwa kwa pamoja kwenye mchezo wa soka.” Alisema Ronaldo alipohojiwa na kituo cha tevisheni cha Sky Sports

Kauli ya Ronaldo ya kutaka kucheza soka kwa miaka 10 ijayo, inadhihirisha wazi amedhamiria kustaafu mchezo huo akiwa na umri wa miaka 41.

Mamadou Sakho Kurudi Ufaransa?
Video: Watu katika miji saba Marekani waandamana kumpinga Trump