Wabunge wanane wa viti maalumu wa Chama cha Wananchi (CUF), walioshinda kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam, wamemuandikia barua Spika wa Bunge, Job Ndugai ya kutaka kurejeshwa kazini.
Wabunge hao wanaomuunga mkono Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, walidaiwa kufukuzwa uanachama wa CUF na Mwenyekiti Prof. Ibrahim Lipumba.
Aidha, Prof. Lipumba anatambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa kama Mwenyekiti halali wa chama hicho na kwa misingi hiyo barua kutoka upande wake ilikubaliwa na Ndugai.
Wabunge hao wamesema kuwa kutokana na hukumu iliyotolewa na Jaji Lugano Mwandambo ambayo iliwarudishia uanachama wao, waliandika barua kwa Spika wa bunge ya kuomba kurudishiwa Ubunge wao.
“Tunaamini kwamba, baada ya mahakama kuu kutenda haki, uamuzi huo naamini utaheshimiwa na tutarejeshewa haki yetu,”amesema Riziki Shahari Mngwai