Aliyekuwa Dada Mkuu shule ya sekondari Jangwani jijini Dar es salaam, Mida Twaha Jumbe ametaja sababu iliyopelekea Shule hiyo kupata matokeo mabovu ya kidato cha sita mwaka 2018 kuwa na kushika nafasi ya tatu kutoka mwisho.

Ametaja sababu hiyo kuwa ni kuwepo ushirikiano hafifu kati ya wanafunzi na walimu na amesema wanafunzi sio wa kulaumiwa kwani kumekuwa na mawasiliano haba kati ya wanafunzi na walimu, umbali kwa wanafunzi wanaoishi nje ya shule ikiwemo mahusiano ya kimapenzi kati ya wafanyakazi wa shuleni hapo na wanafunzi.

“Hakuna mwanafunzi ambaye anataka kufeli masomo na hakuna aliyefurahia matokeo haya maana wanafunzi wengi matokeo yao ya kidato cha nne wamepata division one, two na mzizi wa tatizo ni mfumo wa uongozi wa shule ambao haupo karibu na wanafunzi,” amesema Maida.

Aidha Maida amewashauri walimu kuheshimu kazi yao.

Hata hivyo Jana Naibu Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo ametoa amri kwa maofisa Elimu wa mkoa na wilaya kufanya mabadiliko ya uongozi wa shule hiyo ikiwa pamoja na kufanya uhamisho wa walimu waliofundisha shule kwa zaidi ya miaka mitano.

Thibaut Courtois kumrudisha Petr Cech Chelsea
Pires amponda Arsene Wenger, amkubali Unai Emery