Baada ya Ripoti iliyotolewa na Dar24 Media juu ya shida ya maji katika Kijiji cha Ranchi Kilichopo Mkoani Morogoro, hatimaye Wananchi wa eneo hilo wameonesha kufurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa Kisima cha maji kitakachosaidia kuondokana na adha hiyo.
Ripoti hiyo ilitolewa mapema mwaka huu, baada ya kutembelea eneo hilo lililopo Barabara ya Morogoro – Dodoma, ambapo timu ya Dar24 Media ilishuhudia uwepo wa changamoto ya maji na kujionea jinsi Wananchi wanavyotumia maji hayo kwa kuchangia na Mifugo, hali ambayo haikuwa salama kiafya.
Baada ya ripoti hiyo, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso alielekeza kuanza kwa Ujenzi wa kisima hicho mara moja, huku akiipongeza Dar24 Media kwa kuibua changamoto hiyo na kuomba iendeleze uibuaji wa mambo mengine yatakayosaidia kufanikisha maendeleo ya nchi.
Hata hivyo, Wananchi hao kwa nyakati tofauti wameonesha hisia zao juu ya maendeleo ya ujenzi wa kisima hicho cha maji, huku wakisema kukamilika kwake kutasaidia wao na maeneo jirani kuondokana na shida hiyo ya maji, iliyokuwa ikiwakabili kwa muda mrefu.
Zifuatazo ni picha, zikionesha matukio mbalimbali baada ya Dar24 kufika eneo la tukio Kijijini hapo mapema mwaka huu (2023), na kukuta baadhi ya Wananchi wakichota, kunywa na kufulia maji hayo kwa kuchangia na mifugo.
N hizi Picha zifuatazo, ni baada ya kutoka kwa Ripoti iliyopelekea Waziri wa Maji Juma Aweso kuagiza ujenzi wa kisima cha Maji, na tafadhali kaa tayari kwa ripoti kamili ya hali ilivyo kwasasa juu ya eneo hilo, ambayo itakujia hivi karibuni kupitia akaunti zetu za mitandao ya kijamii za Facebook, Instagram, Twitter na Youtube @dar24media.