Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Basila Mwanukuzi amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga, Bombo baada ya kupata ajali ya gari katika Barabara ya Tanga- Segera eneo la Hale Wilayani Korogwe.

Kaimu RPC wa Tanga, David Mwasimbo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo “Ajali imetokea usiku wa kuamkia leo, Mkuu wa Wilaya anaendelea vizuri isipokuwa Dereva wake hali si nzuri, chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi, Dereva alikuwa anajaribu kuyapita magari mengine na ndipo ajali ikatokea”

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo, Dk Jonathan Gudemo amekiri kuwapokea majeruhi watatu wa ajali hiyo akiwemo DC Mwanukuzi

“Majeruhi wawili hali zao zinaendelea kuimarika akiwemo DC na bado wapo chini ya uangalizi wa matabibu na majeruhi mmoja tumempatia rufaa ya kwenda Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi”amesema Dkt Gudemo

Kauli za Diamond na Zuchu sakata la kufungiwa video ya 'Mtasubiri'
Ripoti ya CAG yampeleka Majaliwa Sengerema; Watumishi 30 mikononi mwa TAKUKURU