Watu watano wamejeruhiwa akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Albert Msando na mwenzake wa Ulanga, Ngolo Malenya baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutokea Mbigiri – Dakawa Wilaya ya Kilosa kuelekea Morogoro Mjini kugongana uso kwa uso na gari dogo aina ya Toyota Land Cruser yenye namba za usajili DFPA 8530 iliyokua ikitokea Morogoro Mjini kueleke Dodoma .

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fotunatus Musilimu amesema kuwa ajali hiyo imetokea eneo la Dakawa, wakati wakuu hao wa wilaya wakiwahi kwenye msafara wa Waziri Mkuu uliokuwa ukitokea kwenye Kiwanda cha Sukari cha Mbigiri, kilichopo Wilayani Kilosa na kuelekea kiwanda cha Nyama cha Nguru Hills Ranch kilichopo Wilayani Mvomero.

Aidha Kaimu Mganga mfawidhi hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro, Dk. Kessy Ngallawa amethibitisha kupokea majeruhiwa hao majira ya saa 7 mchana leo Agosti 14 akiwemo wakuu hao wa wilaya, Dereva wa gari ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro na wauguzi wawili walikua kwenye gari iliyopata ajali.

Hata hivyo Mganga Mfawadhi Dk. Kessy amesema baada ya kupata matibabu ya awali wakuu wa wilaya wamehamishiwa kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibababu.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Augusti 15, 2021
Majaliwa atoa maagizo kwa wasimamimizi wa vituo vya umeme nchini