Mkuu wa wilaya Tunduru, mkoani Ruvuma Julius Mtatiro amewabaini wanafunzi wawili wa darasa la saba katika shule ya msingi Mchangani wakiishi kama mke na mume baada ya shule kufungwa kwa ajili ya ugonjwa wa Corona.

DC Mtatiro amewabaini wanafunzi hao wakati akifanya oparesheni ya kuwafuatilia watoto walioko majumbani katika kipindi hiki cha likizo.

Hata hivyo Kiongozi huyo amemnyoa nywele mwanafunzi huyo wa kiume huku akimuagiza mwalimu Mkuu wa shule hiyo kumchapa viboko ikiwa ni moja ya adhabu.

Dc Mtatiro alituma kikosi chake cha kupambana na mimba kikiongozwa na Mtendaji wa kijiji na Mwalimu mkuu wa shule hiyo, na kubaini wanafunzi hao kuishi kinyumba katika nyumba waliopangishiwa na mzazi wa mtoto kike.

Aidha DC ameagiza wazazi wa watoto hao kukamatwa na hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yao.

OSHA watoa msaada vifaa kinga dhidi ya Corona kwa wasioona
Kilimo chaongoza mchango pato la Taifa 2019